Part One: Jahazi la mapenzi

Part One: Jahazi la mapenzi


Sehemu ya kwanza

Furaha ilikuwa imemtawala chris katika moyo wake, furaha 
ambayo haikuhesabika wala kupimika, mawazo yalimtambaa
 katika akili yake na kuzalisha tabasam pana lililonawili na 
kuchanua katika sura yake mithili ya bustani yenye maua mengi na yenye rangi ya tofauti tofauti zenye kupendeza. Alikuwa barabarani kimwili lakini kiakili alikuwa nyumbani akiongeana mama yake, Janety na Natasha. Aliwaza na kuwazua.. alikili yake ilibishana na ubongo wake na kichwa chake kukawa kama mkutano wa vijana wabishanao kwa mbwembwe juu ya timu zao za zinazoshiriki katika ligi kuu……

.” Bilashaka mama atafurahi sana kunion maana nina miezi  mitatu sijakutana na familia yangu….. oooohhhh mungu wangu na Janety na Natasha lazima watanitaka niwapeleke shopping this week, oooohhh my God…. Lakini sinakazi yoyote wiki hii wala kikao chochote hivyo siwezi kukataa….. tangu baba yangu alipofariki nimekuwa nashughulikia sana mambo ya kifamilia, majukum yameongezeka sana…. Lakini hamna shida kwani sina mke wala watoto wanaonitizama na kunitegemea zaidi ya familia yangu….”

mawazo hayo yaliyumbisha kichwa cha Chris na kumfanya azame katika bahari
 ya viulizo na tabasam. Ghafla alisikia kama kunamtu anagonga kioo cha gari yake, 
kushituka alikuwa ni mototo mdogo aliyekuwa amenyosha mikono yake miliwi kijarubu 
bahati yake kama anaweza kuambulia chochote….. chris alimtizama Yule mototo na
 kugundua kuwa alikuwa ni omba omba…. Alikuwa amevaa kaushi yenye matundu
 yasiyo na idadi kilakona, ilikuwa ni vugumu kutambua rangi halisi ya nguo ile kwani 
nyeupe si nyeupe, nyeusi si nyeusi, udhurungi si udhurungi….. alikuwa amevaa kaptula 
fupi na yenye vilaka vitatu upande wa nyuma, vilaka niwili goti la kushoto na kilaka
kimoja goti la kulia…. Chris aliwaza huenda ni fashion mpya au ni toleo la kaptula 
kutoka suruari aina ya cryz jeans, nywele zakezilikuwa nyekundu na si nyeusi, alio-
nekana vizuri sana tangu ngozi yake mpaka mifupa yake yote, alipauka na kupoteza 
rangi yake ya asili, lakini kutokanana ule uchafu alilazimika kukataa na kupata 
jibu kwamba motto Yule anaishi katika mazingira magumu….  Aliingiza mkono 
mfukoni na kutoa noti ya shilingi elfu tano na kumpa Yule mtoto, 
pembeni alimuona dada mmoja mjamzito ambaye alikuwa na kati ya miaka 23 au 24. 
Alikuwa anatembea kwa kujivuta sana kiasikwamba anatamani alale hapo barab-
arani na kesho aendeleena safari yake…. Alimuonea huruma na kumuita….

“dada habari yako? Unakwenda wapi? 
Yalikuwa ni maswali aliyoulizwa yele mwanadada…  alijibu kwa heshima….
 “naitwa Sabrina na naelekea tabata kimanga” ok mimi na kwenda tabata segerea twende nikupe lift… ok asante sana kaka…. 
Askari wa usalama barabarani alishaanza kuruhusu magari yanayotoka mbezi kuelekea maeneo
 mengine ya jiji la dare s salaam, mazungumzo kati ya chris na sabrina katika gari yalonoga na
 kukolea mithili ya mua uliozamisha meli walicheka na kutabasamu na kubadilisha mawazo… 
Sabrina alikuwa amevaa dira za zambalau na chakavu, alionekana amechoka kiasi kwamba 
amebakiza nusu saa tu aitwe na manesi kwenda kuongeza mwana duniani….. chris hakujali 
hilo alionekana mwingi wa soga ili kumlidhisha mgeni wake aliyekuwa kama mgunjwa mahututi
….. ghafla walifika njiapanda tabata segerea na kuachana pale, chris alimpa Sabrina 
elfu tano na kumwambia achukue bodaboda inayoweza kumfikisha kimanga…. Chris 
alikamata njia na kuanza kuesabu nyumba kadhaa za majirani kabla hajaifikia nyumba yao…. 
Kabla ya kufika kwao alinunua hahitaji kadha wa kadha ambayo yangekuwa muhimu na 
yanahitajika pale nyumbani……… alitoa tabasamu pana alipoona geti kubwa lenye rangi 
nyeusi, miti mirefu na yenye upendeza, maua na bustani nzuri….. alipiga honi na mlinzi 
alifungua geti… alienda na kuegesha gari kando ya bombala maji ili gari yake isafishwe, 
alishuka na koungea mawili matatu na mlinzi Yule…. 

Ghafla neema alitokea…. Neema ni mfanyakazi wa ndani, alimuona chris na akakimbia 
kumpokea kwa kumkumbatia na akadeka dakika tatu kwa chris kabla naye chris kwenda 
kudeka kwa mama yake…. Chris alibaki na kiulizo kimoja na alijiuliza jambo ambalo 
hatayeye hakulipatia ufumbuzi wa papo kwa papo…. “hivi mama, janeth na Natasha 
hawapo au wapo? Mbona hawajaja kunipokea? Au wamelala? Mmmhhhhh lakini…… 
aaahhhh ok nitajua humohumo ndani……” aliondoka na kuelekea ndani ili kuwatizama 
ndugu zake na mama yake aliowapoteza machoni mwake kwa mda wa miezi mitatu…. 
Alifungua mlango alimkuta mama kaka na wadogo zake wamekaa katika kochi kama 
wanajadili bajeti ya nchi ya ulimwengu wa kwanza….. alitabasamu na kuwasalimu ndu-
gu zake….. haikuwa ni kawaida kuwakuta ndugu zake wamamkasilikia kiasi kile hak-
una aliyejibu salamu yake isipokuwa alipokelewa na maneno ambayo hata yeye haku-
jua yanatokea katika karne ya ngapi…. Mama yake alimtazama chris kwa jicho la 
dharau na kampandisha kasha akamshusha pembeni….. chris alibaki amesiamam na sasa
 aliamua kukaachini na kuanza kumuomba radhi mama yake….. ”Mama samahani 
sana nilichelewa kuja kutokana na foleni lakini pia nadhani nilitoa taarifa kwa miezi 
iliyopita kwamba sitafika kutokana na kubanwa na shughuli za kiofisi, mama hata mimi 
napenda sana kuwa pamoja na familia yangu wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki.”  
hakumaliza kuongea akapokelewa na maneno ya uchi toka kwa janeth…. 
“hahahahahaaaaaa aaaaaloooooo…… kaka hivi huna kazi?, huna pesa? Huna gari? Unamiaka 
mingapi sasa eeeehhhh… mtoto yuko wapi? Mke yu wapi? Nguvu unapoteza kwenye 
mashuka au…… unadhani sisi hatupendi mawifi? Eeeehhhhh” aliongea maneno hayo akiwa
 kachachamaa kama amepandwa na mashetani huku vidole vya mikono yake vimejipanga
 kama ndege za kivita katika maadhimisho ya siku ya mashujaa…. Chris alionekana amejishika 

kichwa na ameinama chini…. Ghafla Tayana alidakia alipoishia janety na akaanza kumpasha 
kwa maneno yaliyojaa uchungu na ukakasi, maneno makali kama pilipili yasiyo lika au hata kulambika….. 
“…..hivi huoni huko njiani unapopita warembo wa kuwaoa au, huigi rafikizako wanapocheza na watoto wao au wewe umeridhika kucheza na mito, kaka sema mapema kama jogoo hawiki twende kwa sangoma, vipiiiiii eeehhhh kaka uwezi kupanda mlima, huwezi kuvuna nazi, we domo zege au ndo uji wa majimbi unakupelekeshaaaaa…. Kama huwezi sema bwanawewe tukufungashie mwakuishi nae maana we si huoni aaaahhhhh miaka 26 sasa huna hata dalili aaaaaahhhhh au unataka mwanao aje kukuita babu na sio baba semaaaaaaa…..” 
yalikuwa ni maneno yaliyomuumiza sana chris aliwaza na kuwazua kasha akamtazama
 mama yake aliyekuwa akimtizma kwa jicho la upande kasha akaamua kutoa kauli yake 
pia….. 
mwanangu unanini wewe marangapi nakwambia uoe hutaki? Mbona sikuelewi? Au umekuwa hanithi sema baba yangu ili tukazulule kwa wataalam khaaaaaa janga gani tena hili……” 
chris alidondosha machozi mfurulizo na akaamua kutoka nje na akamuita mfanyakazi 
wa ndani ambaye ni neema…………….
Itaendelea……

Kwa ushauri, maoni na mapendekezo wasiliana na mwandishi na mmiliki wa simulizi kupitia:-
0658840321 / 0765483200 / 0624804059

Au niandikie kupitia e-mail yangu

scotchonal rox @instagram na Raphael kajuni @facebook.



share this article to: Facebook Twitter Google+ Linkedin Technorati Digg
Posted by Slaustz, Published at May 03, 2017 and have 0 comments

No comments:

Post a Comment

close