THE HISTORY OF "NI SALAMA ROHONI MWANGU" SONG

THE HISTORY OF "NI SALAMA ROHONI MWANGU" SONG

HISTORIA YA WIMBO  
"NI SALAMA ROHONI MWANGU"

Wimbo wa "Ni Salama Rohoni Mwangu" ulitokana na mikasa iliyomkuta  mwanasheria na wakili mahiri mkristo aliyeitwa Heratio Spafford. Alikuwa na watoto watano akiwemo wa kiume mmoja. Mwanae pekee wa kiume alifariki mwaka 1871 akiwa na miaka minne.

Mwaka 1872 kulizuka moto mkubwa sana maarufu kama moto mkubwa wa Chicago ambao uliteketeza shamba na majumba yake, vitu alivyokuwa amejipatia kwa fedha alizoingiza kutokana na umahiri wake katika taaluma na kazi yake.

Mwaka 1873 alitanguliza  mkewe na mabinti zake wanne kwenda mapumziko Ulaya ambapo angewafuata kesho yake baada ya kumaliza kazi alizokuwa nazo.

Meli iliyokuwa ikiitwa Ss Ville du Havre iliyobeba familia yake ilizama na binti zake wote walifariki akapona mkewe tu ambaye alimtumia  telegramu *Nimepona mimi tu*.

Akiwa njiani kurudi nyumbani kwake nyumba ilimokuwa ofisi yake ikaungua. Kwa bahati nzuri nzuri alikuwa ameikatia bima lakini kampuni ya bima ilikataa kumlipa kwa madai kuwa lile lilikuwa  janga la asili (An Act of God).  Heratio alibaki mtupu - hana pa kuishi wala hana fedha. Akiwa ni mtu wa kiroho aliyemtegemea Mungu alikaa akitafakari yale yaliyokuwa yakitokea katika maisha yake na ndipo alipochukua kalamu na karatasi na kuandika *"Lolote liwalo, Bwana wangu, umenifundisha kusema - Ni salama rohoni mwangu*".  (Maandishi mengine yanasema aliandika maneno haya alipofika eneo la bahari ilipozama meli akiwa safarini kumfuata mkewe Ulaya). 

Baadae maneno haya yaliongezwa mashairi na kutiwa muziki na kuwa wimbo maarufu sana na wenye mguso wa kipekee wa *Salama Rohoni*. Kama ilivyokuwa kwa Ayubu Heratio alikuja kuinuliwa akapata watoto wengine na mali na fedha.
ulikosa hii ya uzinduzi wa victor katumaku
Asante kwa kuitembelea website yetu. Kalibu tena.





share this article to: Facebook Twitter Google+ Linkedin Technorati Digg
Posted by Slaustz, Published at July 02, 2017 and have 0 comments

No comments:

Post a Comment

close