New Audio;HB staizer Ft jay 4 - Wako wapi

New Audio;HB staizer Ft jay 4 - Wako wapi

Naitwa Hamis juma, ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu wa mzee juma. Nimepata elimu yangu ya sekondari na ya msingi huko mkoani shinyanga. Sasa ni mwanachuo chuo cha DUCE.

Mbali na masomo yangu,Katika maisha yangu nimepitia vitu vingi vya kuhangaika hapa na pale ili mradi maisha yaende. Nimeanza rasmi harakati za kufanya muziki toka mwaka 2013 japokua hapo nyuma kipaji kilikuwepo lakini sikukitilia maanani sana hii inatokana na wanajamii ambao walikua wananizunguka kutopenda sanaa. 

Baada ya kujichanganya na jamii tofauti ndipo nikagundua kipaji kilichomo ndani yangu. Sifanyi music kwa sababu basi tu lakini nafanya kwa sababu ndicho kitu nnachokipenda. Lengo langu kubwa ni kuja kufikia level za juu na kufanya poa sana ndani ya nchi hata nje pia. 

Muziki unahitaji jitihada sana ili uweze kutusua lakini muziki bila mashabiki pia so kitu, nawaomba mashabiki zangu na wengine waendelee kusapoti muziki wangu kwani bila wao Mimi so kitu. Pia salute sana kwa wana wanaosapoti muziki 



share this article to: Facebook Twitter Google+ Linkedin Technorati Digg
Posted by Slaustz, Published at July 02, 2017 and have 0 comments

No comments:

Post a Comment

close